Shule ina maktaba bora yenye vitabu vya kutosha kwa kila somo. pia maktaba yenye mazingira bora na tulivu kwa wanafunzi na walimu kujisomea wakati wowote .
Shule ina maabara bora sana kwa masomo ya sayansi. pia imejaa vifaa vya kutosha kwa masomo yote matatu ya sayansi physics , Biology na Chemistry
Shule inapatikana katika mazingira tulivu sana, yaliyo kimya na yanayofaa kwa watoto wa kike kujisomea
Shule inawajenga watoto katika imani ya bwana bila kubagua imani ya mtu. pia kumwabudu mungu wakati wote
Shule ina maabara bora kabisa yakufundishia Kompyuta ili kuwafanya wanafunzi kuijua teknolojia ili kuendena na maisha ya kisasa na ushindani.
shule inapatikana katika mitandao mbali mbali ya kijamii kama| Facebook kupitia michaud page
wanafunzi wanafundishwa somo la kompyuta kwa vitendo, Kwa madarasa yote.
Masomo ya preform one yanafundishwa shuleni kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Septemba hadai Disemba kila mwaka, Wanafunzi hupewa huduma zote kama wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne
Wanafunzi wanafundishwa masomo ya sayansi kwa vitendo ili kuwapa uwezo na ubunifu wa kufanya vitu mbali mbali vya kisayansi bila kujali jinsia zao
Wanafunzi wanajengewa uwezo wa kuongea na kuandika lugha ya kiingereza kwa usahihi. sambamba na hilo wamekuwa wakishindana na kushida mashindano mbalimbali ya kuandika na kuongea kiingereza